Kwa mujibu wa kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, kikinukuu Al-Maalumah, chanzo hicho cha Syria kimefichua yaliyokuwa nyuma ya pazia ya mkutano wa siri wa kiusalama wa ngazi ya juu, ambao ulisababisha kufikiwa makubaliano ya kuwafundisha na kuwahamisha maelfu ya mamluki kutoka katika makundi yenye silaha ya Syria kwa ajili ya kushiriki katika vita vya Yemen.
Chanzo hicho kimesema: Mkutano huo wa siri wa kiusalama uliwahusisha maafisa wa usalama wa Marekani pamoja na Tom Barrack, mjumbe wa Rais wa Marekani, na maafisa wa usalama kutoka Saudi Arabia na Uturuki. Kwa upande wa Syria, walihudhuria Ali al-Naasan, Mkuu wa Majeshi ya Syria, Asaad al-Shaibani, Waziri wa Mambo ya Nje, pamoja na mtu anayejulikana kwa jina la Abu Bakr al-Homsi.
Chanzo hicho kiliongeza kuwa; washiriki walikubaliana kuwahamisha kwa awamu mamluki 3,500 kutoka katika makundi yenye silaha ya Syria kwenda Yemen. Kundi la kwanza litakuwa na wapiganaji 1,200, huku waliobaki wakitumwa katika awamu mbili zinazofuatana.
Chanzo hicho kilifafanua kuwa mpango wa uhamishaji ni kwamba wapiganaji hao wenye silaha watahamishwa kutoka katika viwanja vya ndege vya Syria kwenda Ankara, kisha kutoka Uturuki watapelekwa Saudi Arabia kwa kutumia kifuniko cha madai kwamba ni “watalii”, ili waweze kupewa vifaa na silaha kikamilifu na upande wa Saudi Arabia.
Chanzo hicho kilieleza pia kuwa; kabla ya mamluki hao wa Syria kupelekwa rasmi katika medani za mapigano nchini Yemen, watapatiwa mafunzo makali ya kijeshi na maafisa kutoka Uturuki na Azerbaijan, ndani ya ardhi ya Saudi Arabia.
Maoni yako